Mon, Jan 19, 2026
  Email: info@kist.ac.tz    
KONGAMANO LA MIAKA 62 YA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR.
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), kupitia Serikali ya Wanafunzi ya Taasisi ya Karume (KISTSO), leo tarehe 11/01/2026, wamefanya Kongamano la kumbu kumbu ya miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Katika kongamano hilo mada mbali mbali zilitolewa ikiwemo Historia ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Nafasi ya Vijana Wasomi katika kuyaenzi Mapinduzi kwa kutunza amani kwa Vitendo, Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar pamoja na Ubunifu wa Vijana katika nguvu mpya ya Mapinduzi ya kisasa.
Kongamano hilo Lilihudhuriwa na Mbunge wa Viti Maalumu Kundi la Vyuo vikuu Mhe. Dkt. Zeyana Hamid, Katibu kutoka Idara ya Organization ya Vijana Bw. Mrakibu Mbarouk , Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), Dkt. Mahmoud Abdulwahab Alawi, Katibu Mkuu Mstaafu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Idrissa Muslim Hijja, Mtoa mada ya Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar Bw. Mzee Kombo pamoja na Wageni waalikwa kutoka Sehemu mbali mbali wakiwemo Wanafunzi, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Idrissa Muslim Hija katika Taasisi ya Karume Mbweni Zanzibar.
Kongamano la kumbu kumbu ya Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hufanyika kila mwaka katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), katika kipindi cha kuelekea kuadhimisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa lengo la kuwakumbusha Vijana kuhusu umuhimu wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.