TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), inatangaza nafasi tisa (09) za kazi, moja (01) kwa kada ya Taaluma na nane (08) kwa kada za Utawala katika Idara zifuatazo:
A. IDARA YA ELEKTRONIKI, MAWASILIANO YA ANGA NA KOMPYUTA
(ELECTRONIC, TELECOMMUNICATION AND COMPUTER ENGINEERING DEPARTMENT) - NAFASI (01) UNGUJA
1. MKUFUNZI DARAJA LA II - NAFASI (01) - KITUO CHA KAZI UNGUJA
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe amehitimu Shahada ya Uzamili katika moja ya fani zifuatazo:
- Information and Communication Technology with Business
- Information and Communication Technology with Accounting
- Information Technology
- Computer Science
- Computer Engineering
- Information System
- Computer Information Security na fani zinazofanana na hizo, kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
- Awe Mzanzibari asiezidi miaka arubaini na tano (45)
- Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
- Awe na ufaulu usiopungua CGPA 4.0 kwa shahada ya uzamili (Master degree) na CGPA 3.5 kwa Shahada ya kwanza (Bachelor Degree)
- Mshahara sawa na ngazi ZPSK - 08
MAJUKUMU YA KAZI ZA MKUFUNZI
- Kufundisha katika ngazi ya Shahada
- Kufanya tafiti, kutoa ushauri elekezi na kutoa huduma kwa jamii
- Kufanya kazi nyengine ambazo atapangiwa na Mkuu wake wa kazi
B. IDARA YA SAYANSI (SCIENCE DEPARTMENT) - NAFASI MOJA (01)
1. AQUATIC TECHNICIAN - NAFASI (01) - KITUO CHA KAZI UNGUJA
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe amehitimu Stashahada katika moja ya fani zifuatazo:
- Aquatic Product Processing Technology
- Aquaculture
- Aquatic Ecology
- Fish Biology and Taxonomy
- Fisheries Resources Management Science
- Laboratory Technology na fani zinazofanana na hizo, kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
- Awe Mzanzibari asiezidi miaka arubaini na tano (45)
- Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
- Mshahara sawa na ngazi ZPSF - 05
C. IDARA YA UHANDISI UMEME (ELECTRICAL ENGINEERING DEPARTMENT)
1. ELECTRICAL TECHNICIAN NAFASI (02) - KITUO CHA KAZI PEMBA
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe amehitimu Stashahada katika moja ya fani zifuatazo:
- Electrical Engineering
- Electrical and Electronics Engineering
- Electrical with Renewable Energy Engineering na fani zinazofanana na hizo, kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
- Awe Mzanzibari asiezidi miaka arubaini na tano (45)
- Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
- Mshahara sawa na ngazi ZPSF - 05
D. IDARA YA UHANDISI UJENZI NA USAFIRISHAJI (CIVIL AND TRANSPORTATION ENGINEERING DEPARTMENT) - NAFASI TATU (03)
1. CIVIL TECHNICIAN - NAFASI (02) KITUO CHA KAZI UNGUJA
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe amehitimu Stashahada ya Civil Engineering au fani zinazofanana na hiyo, kutoka katika Vyuo vinavyotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
- Awe Mzanzibari asiezidi miaka arubaini na tano (45)
- Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
- Mshahara sawa na ngazi ZPSF - 05
2. PLUMBER TECHNICIAN - NAFASI (01) KITUO CHA KAZI UNGUJA
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe amehitimu Astashahada ya Plumber au fani zinazofanana na hiyo, kutoka katika Vyuo vinavyotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
- Awe Mzanzibari asiezidi miaka arubaini na tano (45)
- Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
- Mshahara sawa na ngazi ZPSD - 07
E. IDARA YA UHANDISI MITAMBO NA USAFIRI WA ANGA (MECHANICAL ENGINEERING AND AVIATION DEPARTMENT) - NAFASI (02)
1. AUTOMOTIVE TECHNICIAN - NAFASI (01) KITUO CHA KAZI UNGUJA
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe amehitimu Astashahada katika moja ya fani zifuatazo:
- Automotive Engineering
- Automobile Engineering
- Motor vehicle Mechanics
- Vehicle Maintenance and repair
- Automotive Engineering Technology
- Auto-electrical Engineering au fani zinazofanana na hizo, kutoka katika Vyuo vinavyotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
- Awe Mzanzibari asiezidi miaka arubaini na tano (45)
- Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
- Mshahara sawa na ngazi ZPSD - 07
2. WELDING TECHNICIAN - NAFASI (01) KITUO CHA KAZI UNGUJA
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe amehitimu Astashahada katika moja ya fani zifuatazo:
- Welding and Metal Fabrication
- Welding and Fabrication Engineering
- Manufacturing Engineering Technology
- Mechanical Engineering au fani zinazofanana na hizo, kutoka katika Vyuo vinavyotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
- Awe Mzanzibari asiezidi miaka arubaini na tano (45)
- Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
- Mshahara sawa na ngazi ZPSD - 07
MAJUKUMU YA UJUMLA YA KAZI KWA TECHNICIANS
- Kupanga vifaa vyote vya maabara katika mpango maalum
- Kuhakikisha kuwa maabara zinakuwa safi na salama kwa ajili ya matumizi
- Kupanga vifaa na vyombo vitakavyotumika kwa ajili ya somo la vitendo
- Kuhakikisha kuwa mashine zote zinafanyiwa matengenezo kwa muda unaostahiki
- Kutekeleza majukumu mengine atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi
JINSI YA KUFANYA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kwa anuani ya:
Mkuu wa Taasisi,
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume,
S. L. P. 467
Zanzibar
Kupitia mfumo wa kielektroniki wa maombi ya ajira (Zanajira) wa Serikali wenye anuani ifuatayo: www.zanajira.go.tz kuanzia tarehe 24 Mei, 2025 hadi tarehe 07 Juni, 2025.
Tangazo hili pia linapatikana katika tovuti ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume yenye anuani www.kist.ac.tz
Maelezo:
- Muombaji ahakikishe anaambatanisha viambatisho vinavyohitajika kwa usahihi
- Muombaji aliesoma nje ya Tanzania atalazimika kufanya uhakiki wa vyeti vyake katika Tume ya Vyuo Vikuu vya Tanzania (TCU)
- Muajiriwa wa Serikali atalazimika kupitisha maombi kwa Muajiri wake kwa kupata ridhaa