UONGOZI WA TAASISI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA KARUME (KIST) UMEPOKEA UGENI KUTOKA KAMPUNI YA BENEDUCE YA NCHINI BRAZIL

2025-11-21 05:24:30 category

Uongozi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST) Umepokea ugeni kutoka Kampuni ya BENEDUCE ya nchini Brazil inayojishughulisha na Ujenzi wa Nyumba zisizotumia matofali.

 

Ujumbe huo uliueleza Uongozi wa Taasisi kuwa Kampuni ya BENEDUCE ipo tayari kushirikiana na Taasisi ya Karume kwa lengo la kutoa ujuzi wa kujenga Nyumba zisizotumia matofali ambazo zitakuwa na faida kubwa hasa katika utunzaji wa mazingira.