Thu, Jan 02, 2025
  Email: info@kist.ac.tz    
Phone:   +255 712-779-267    
Timu ya Mpira wa miguu ya Wafanyakazi kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), imewachapa vikali Timu ya Serikali ya Wanafunzi KISTSO.
Mchezo huo ulikuwa na upinzani mkubwa sana na kuleta matokeo ya 2:0, ambapo Timu ya WAFANYAKAZI WA TAASISI YA KARUME imepata ushindi wa magoli 2 na Timu ya SEREKALI YA WANAFUNZI KISTSO imeangulia 0.
lengo la Mchezo huo ni kumuaga Mkufunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), ambae pia ni Mwalimu wa Michezo katika Taasisi ya Karume. Bw. Walid Kassim Mohammed, ambaye anamaliza muda wake wa utumishi.
Mchezo huo wa Mpira wa Miguu ulifanyika katika Uwanja wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), uliopo Mbweni Zanzibar.