UONGOZI WA TAASISI YA KARUME UKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA UONGOZI WA TUME YA TAIFA YA UNESCO

2025-10-21 06:07:35 category

Uongozi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), umepokea ugeni kutoka Tume ya Taifa ya UNESCO.

 

Lengo la ugeni huo ni kuja kujitambulisha katika Taasisi ya Karume na kuelezea kazi wanazofanya katika Tume hiyo.

 

Tume ya Taifa ya UNESCO ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa lengo la Kupanga, Kuratibu na kusimamia kazi zote za UNESCO nchini Tanzania.