KIST YASAINI HATI YA MAKUBALIANO OBUDA UNIVERSITY.

2026-01-28 09:06:47 category

Tarehe 27/01/2026, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya karume (KIST) imesain hati ya makubaliano  na Chuo Kikuu cha Obuda (Obuda University) Nchini hungary budapest, lengo likiwa ni mashirikiano ya pamoja katika suala zima la Kitaaluma, hati ya makubaliano imesainiwa na Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST) Dkt. Mahmoud Abdulwahab Alawi pamoja na Mkuu wa chuo Kikuu cha Obuda Prof  Levente Kovacs.

 

Mashirikiano hayo yanatarajiwa kuleta manufaa mengi baina ya Taasisi hizo mbili ikiwemo  kubadilishana wataalamu, kutoa nafas za ufadhili, ubunifu pamoja na utafiti.