Tue, Feb 10, 2026
  Email: info@kist.ac.tz    
Tarehe 27/01/2026, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya karume (KIST) imesain hati ya makubaliano na Chuo Kikuu cha Obuda (Obuda University) Nchini hungary budapest, lengo likiwa ni mashirikiano ya pamoja katika suala zima la Kitaaluma, hati ya makubaliano imesainiwa na Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST) Dkt. Mahmoud Abdulwahab Alawi pamoja na Mkuu wa chuo Kikuu cha Obuda Prof Levente Kovacs.
Mashirikiano hayo yanatarajiwa kuleta manufaa mengi baina ya Taasisi hizo mbili ikiwemo kubadilishana wataalamu, kutoa nafas za ufadhili, ubunifu pamoja na utafiti.