KIST YAPOKEA UGENI KUTOKA CHUO KIKUU CHA MTUCI
Uongozi wa Tasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume KIST) umekutana na kufanya mazungumzo ya pamoja na Chuo kikuu cha Moscow Technical University of Communications and Informatics (MTUCI) kilichopo nchini Russia, Kwa lengo la kuanzisha mashirikiano katika suala zima la Kitaaluma.
Katika mazungumzo hayo pande zote mbili zimejadili fursa za ushirikiano katika nyanja za elimu pamoja na dhamira ya kujenga ushirikiano utakaosaidia kukuza ubora wa elimu pamoja na kuimarisha maendeleo ya teknolojia.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 05 Machi 2026, katika Ofisi ya Mkuu wa Tasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume KIST) Mbweni Zanzibar.