TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA NAIBU MKUU TAALUMA

2026-01-20 13:29:01 category

TANGAZO LA KAZI KWA NAFASI YA UONGOZI UTANGULIZI

Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST) inatangaza nafasi moja (01) ya kazi kwa nafasi ya Uongozi wa Taasisi, kama ifuatavyo: -

1.0 NAIBU MKUU WA TAASISI – TAALUMA, UTAFITI, UBUNIFU NA USHAURI ELEKEZI

SIFA ZA MUOMBAJI

1. Awe Mzanzibari mwenye kitambulisho halali cha Mzanzibari Mkaazi.

2. Awe na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani ya Sayansi na Teknolojia, au Uhandisi kutoka katika Chuo, kinachotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Awe na uzoefu wa Uongozi na Utawala wa angalau miaka mitatu (3) katika Taasisi ya Kitaaluma.

4. Awe mbunifu, mwenye uzoefu wa kufanya tafiti, kuchapisha makala katika majarida yanayotambulika, pamoja na kutoa ushauri elekezi wa kitaaluma.

 

KAZI NA MAJUKUMU

1. Atakuwa Mshauri Mkuu wa Taasisi katika masuala ya Taaluma na mambo yote ya kitaaluma.

2. Kuwasilisha matokeo ya mitihani katika Bodi ya Taaluma na Baraza la Taasisi.

3. Kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Taasisi pamoja na miongozo husika.

4. Kusimamia Idara zilizo chini yake.

5. Atakuwa kiungo kati ya Idara mbalimbali.

6. Kuwasilisha ripoti za matokeo ya kila muhula kwa mamlaka husika.

 

NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao yakiwa yamefungwa vizuri kwenye bahasha na kuambatanisha nyaraka zifuatazo: -

a) Barua ya maombi inayoonesha wazi nafasi anayoiomba pamoja na Wasifu binafsi (CV) nakala sita (06).

b) Vivuli vya vyeti vya masomo na matokeo yake.

c) Vyeti vya masomo vilivyopatikana nje ya nchi lazima vithibitishwe na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

d) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.

e) Majina ya wadhamini watatu (03), anuani zao za mawasiliano pamoja na taarifa za siri za tathmini ya mwombaji.

f) Picha tatu (03) za pasipoti zilizopigwa karibuni.

g) Namba ya simu na anuani ya barua pepe (e-mail).

h) Vivuli vitatu (03) vya Kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi.

 

TANBIHI

1. Nafasi ya Naibu Mkuu wa Taasisi ni ya mkataba wa miaka mitatu (03) na inaweza kuongezwa kwa kipindi chengine cha miaka mitatu (03) kwa mujibu wa Sheria ya Taasisi.

2. Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni Siku ya Jumanne tarehe ya 03/02/2026 Saa 9:30 alasiri katika Taasisi ya Karume na kwa njia ya barua pepe ni saa sita 6 :00 kamili usiku.

3. Maombi yawasilishwe moja kwa moja katika Masjala ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume ndani ya saa za kazi, au kupitia barua pepe info@kist.ac.tz .

4. Mawasiliano yatafanywa kwa waombaji watakaokidhi vigezo pekee (shortlisted).

5. Maombi yote yawasilishwe kwa anuani ifuatayo:-

MKUU WA TAASISI

Taasisi Sayansi na Teknolojia ya Karume 

S.L.P 476

E-mail: info@kist.ac.tz

Zanzibar