Recent News

KIST YAPATA UGENI KUTOKA PEMBA.

2023-10-05 13:12:18 category

Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), wametembelewa na Vijana wa hamasa kutoka Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kusini Pemba.

Vijana hao wamefika katika Taasisi ya Karume kwa lengo la kufanya ziara ya Utalii wa ndani ili kujifunza mambo mbali mbali katika Taasisi hiyo ikiwemo Bustani.

 Pia wamepata fursa ya kujuwa historia ya Taasisi ya Karume pamoja na Fursa mbali mbali zinazopatikanwa KIST.