KIST YAPOKEA UGENI KUTOKA CHUO CHA AFYA NA TEKNOLOJIA ZANZIBAR

2026-04-02 12:39:24 category

Uongozi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST) leo tarehe 02/04/2026, umepokea ugeni kutoka Chuo cha Afya na Teknolojia Zanzibar (Zanzibar College of Health and Technology) kilichopo Chukwani nje kidogo na Mji wa Zanzibar.

 

Lengo la ugeni huo ni kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya kitaaluma, hususan katika nyanja za Sayansi na Teknolojia.

 

Ugeni huo ulipata nafasi ya kutembelea Workshop mbalimbali za Taasisi ya Karume na kupata maelezo kuhusu Vifaa mbali mbali vilivyomo katika Workshop hizo.

 

Ziara hiyo imeimarisha ushirikiano kati ya Vyuo hivo, pamoja na kufungua fursa za kujifunza za kitaaluma kwa Wakufunzi kupitia kubadilishana maarifa na uzoefu.

 

Uongozi wa KIST umeeleza kufurahishwa na ujio huo na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano kwa manufaa ya Sekta ya elimu na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.