Tue, Jan 28, 2025
  Email: info@kist.ac.tz    
Phone:   +255 712-779-267    
Wawakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la uwekezaji rasilimali watu (GFP), linalojishuhulisha na masuala ya uchomeaji (Welding) Kutoka Nchini Marekani wamefika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), kwa lengo la kuweka ushirikiano katika elimu ya ufundi.
GFP inalengo la kuanzisha kituo cha umahiri wa uchomaji vyuma ili kuzalisha wataalamu wanaotambulika kitaifa na kimataifa katika nyanja ya uchomeaji vyuma (Certified Welding Engineer).
Pia walipata fursa ya kutembelea workshop mbalimbali za Taasisi ili kujionea vifaa vya kufundishia.