TAASISI YA KARUME YAENDELEA NA MASHIRIKIANO YA KITAALUMA

2025-01-28 06:48:08 category

Wawakilishi kutoka German University Technology nchini Oman, wamefika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), na kuonana na Uongozi wa Taasisi hiyo, kwa lengo la kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa Kitaaluma.

German University Technology kwa kushirikiana na Taasisi ya Karume wanampango wa kutoa elimu pamoja na kuandaa Warsha (WORKSHOP) kuhusu kuhifadhi na kuendeleza Miji Mikogwe nchini, ambapo wataalam mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki warsha hiyo.

Wawakilishi hao wamefanya mazungumzo na Uongozi wa Taasisi ya Karume leo Tarehe 27/01/2025, katika Ofisi ya Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), Mbweni Zanzibar.