Thu, Apr 03, 2025
  Email: info@kist.ac.tz    
Phone:   +255 712-779-267    
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imesema imerizishwa na utekelezaji wa Miradi ya Majengo yaliyojegwa katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Kamati hiyo imeyasema hayo ilipofika katika Taasisi ya Karume kwa lengo la kukaguwa Miradi hiyo pamoja na kupata maelezo ambayo yanaeleza utekelezaji wa miradi hiyo iliyosimamiwa na KIST hadi kukamilika kwake.
Miongoni mwa Miradi hiyo iliyojegwa ni Jengo la Utawala la Taasisi ya Karume, Jengo la Hanga pamoja na Maabara ya Sayansi ya Karume.