Fri, Apr 04, 2025
Email: info@kist.ac.tz
Phone: +255 712-779-267
TAASISI ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), inaendelea kupokea wageni kutoka Kampuni mbali mbali nchini, kwa lengo la kuzidisha kuweka mashirikiano katika masuala tofauti ya kimaendeleo yanayofanywa na Taasisi hiyo.
Leo Uongozi wa KIST umepokea Ugeni kutoka Kampuni ya ORYX GAS kwa lengo la kukaa pamoja na kufanya mazungumzo kuhusu mashirikiano katika suala zima la kuendeleza matumizi ya Gesi asilia Zanzibar.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), iliopo Mbweni Zanzibar.
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), imesema itaendelea kuzidi kushirikiana na Kampuni mbali mbali ndani na nnje ya nchi kwa lengo la kuzidi kuleta maendeleo nchini.