Wed, Feb 11, 2026
  Email: info@kist.ac.tz    
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mheshimiwa Khadija Salum Ali, ametembelea Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara zake za kikazi za kukagua na kujionea utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Naibu Waziri alipata fursa ya kutembelea Labo mpya ya Sayansi katika Taasisi hiyo pamoja na kupata maelezo kuhusu programu za kitaaluma zinatolewa sambamba na mchango wa KIST katika kukuza Elimu ya Teknolojia na Ubunifu nchini.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha usimamizi, kuongeza ufanisi wa utoaji wa elimu ya juu na kuendelea kuimarisha Sayansi na Teknolojia Nchini.