KIST YAENDELEA KUKUZA USHIRIKIANO NA VYUO VIKUU

2025-03-13 08:22:37 category

Ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Nanjing University of Aeronautics and Austronautics (NUAA), umefika kwa mara pili katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), kwa lengo la kujadili namna ya Kuendeleza Ushirikiano wa Kitaaluma baina ya Chuo hicho na Taasisi ya Karume.

 

Katika Ujio huo wawakilishi kutoka NUAA waliueleza Uongozi wa Taasisi fursa za masomo zinazopatikana katika Chuo hicho kilichopo nchini China katika ngazi mbalimbali za masomo.

 

Kwa upande wa Uongozi wa Taasisi ya Karume ulisisitiza na kuutaka ujumbe huo kuweka mkazo zaidi katika kuimarisha ushirikiano katika fani mbalimbali zinazofundishwa na Taasisi ya Karume zikiwemo fani zinazohusiana na mambo ya anga , pamoja na kozi mpya zinazotarajiwa kuanzishwa ikiwemo DATA SCIENCE na ARTIFICIAL INTELIGENCE (AI), ili kupata ujuzi na uzoefu wa kutosha kwa lengo la kutoa elimu iliyo bora.