KIST YAPOKEA UGENI KUTOKA BRAZIL

2025-09-22 12:24:03 category

Leo Tarehe 22/09/2025, Uongozi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), Umepokea ugeni kutoka Kampuni ya Tecle Motos Rio ya nchini Brazil inayojishuhulisha na masuala ya Magari ya Umeme.

 

Lengo la ugeni huo ni kufanya mazungumzo na uongozi wa Taasisi ya Karume kuhusu namna ya  kushirikiana katika suala zima la Sekta ya Usafiri ukiwemo usafiri wa Magari ya umeme.

 

Ambapo ilikubaliwa kuwa Taasisi hizi mbili zitashirikiana katika masuala ya Mafunzo ya Utengenezaji wa Magari, Pikipiki, Bajaj na Boti za Umeme kwa lengo la kuhakikisha huduma hiyo inafanyika hapa Nchini.