Thu, Apr 03, 2025
  Email: info@kist.ac.tz    
Phone:   +255 712-779-267    
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), imekutana na kufanya Mazungumzo na wawakilishi kutoka Kitengo cha Ushauri na Utafiti katika Chuo kikuu Cha Hame University of Applied Science (HAMK) cha Nchini Finland, kwa lengo la kukuza Ushirikiano wa kitaaluma hasa katika upande wa Mafunzo ya Ufundi.
Katika Mazungumzo hayo washauri hao walitaka kukusanya maoni kuhusu uendeshaji wa Mafunzo ya Ufundi katika Taasisi ya Karume, kwa lengo la kupata taswira nzima ya utoaji wa Mafunzo hayo ili kuweza kukusanya taarifa na maoni ya kuandaa mapendekezo ya Mradi utakaosaidia Uendeshaji mzuri zaidi wa Mafunzo ya Ufundi.
Uongozi wa Taasisi ya Karume uliwaeleza washauri hao kuwa Taasisi ipo tayari kushirikiana na Chuo hicho katika kuendeleza utoaji mzuri wa mafunzo ya Ufundi hasa kwa kuzingatia mazingira na fursa zilizopo katika nchi yetu.
Aidha Uongozi uliwaeleza wawakilishi hao kuwa Taasisi pia ipo tayari kushirikiana katika ngazi zote za elimu ikiwemo katika fani mpya zilizoanzishwa za Ualimu wa Ufundi.