Mon, Mar 31, 2025
  Email: info@kist.ac.tz    
Phone:   +255 712-779-267    
TAASISI ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), kupitia Idara ya Umeme, leo tarehe 21/02/2025, imefunga mafunzo kuhusu utumiaji wa Vifaa mbali mbali vya kufundishia Wanafunzi wanaosoma fani ya Electrical and Biomedical Engineering.
Mafunzo hayo yametolewa na Profesa Daniel Lawrence Schuster kutoka Taasisi ya BETA Aid (Biomedical Engineering Technology Aid) iliopo nchini Marekani, ambapo mafunzo hayo yamefanyika katika Workshop ya Electrical and Biomedical Engineering katika Taasisi ya Karume Mbweni Zanzibar.
Jumla ya Wakunzi watano (5), wamepata mafunzo hayo na kupatiwa Vyeti vya Ushiriki wa Mafunzo ambayo yaliendeshwa kwa muda wa wiki mbili.