Tue, Apr 14, 2026
  Email: info@kist.ac.tz    
Uongozi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST) leo, tarehe 13 Aprili 2026, umepokea ugeni kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Tanzania Bara, uliyoambatana na wenyeji wao kutoka Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar.
Lengo kuu la ugeni huo ni kufanya mazungumzo kuhusu namna bora ya kuboresha na kuendeleza Kituo cha Ubunifu wa TEHAMA cha Taasisi ya Karume (KIST Innovation Hub).
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufungua fursa mpya za Ubunifu, kuimarisha matumizi ya Teknolojia za kisasa, na kuongeza mchango wa Taasisi katika kukuza Uchumi wa Kidijitali nchini.
Ugeni huo unaonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kuendeleza Sekta ya TEHAMA, pamoja na kuibua vipaji na mawazo mapya yatakayochochea maendeleo endelevu ya Taifa.