Tue, Mar 17, 2026
  Email: info@kist.ac.tz    
Wawakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia Watoto Duniani (UNICEF) wamefika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya karume (KIST) na kuonana na Uongozi wa Taasisi hiyo.
Lengo la ujio huo ni kujitambulisha na kutaka kujuwa mambo mbali mbali kuhusu Taasisi ya karume katika suala zima la elimu ya sayansi na teknolojia.
Taasisi ya Karume imesema wanamashirikiano mazuri na Mashirika mbali mbali ya kimataifa na kushiriki katika shughuli tofauti za kimaendeleo yakiwemo maonesho ili kuonesha ubunifu wa Wanafunzi , hasa katika nyanja za kidijitali.
Miongoni mwa Wawakilishi waliyofika katika Taasisi ya Karume ni Bw. Alfred Mukasa ambae ni Mkuu wa Kitengo cha Athari za Kidijitali na Ubunifu kutoka Ofisi ya UNICEF Tanzania.