News

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

ALI SULEIMAN

 

 

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

 

Taasisi ya Karume inatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:

 

 1. KUJAZA NAFASI TUPU YA MKUFUNZI KATIKA FANI YA MECHANICAL ENGINEERING DARAJA LA II AU MWANDAMIZI DARAJA LA PILI NAFASI MOJA (1).

     Sifa za kuajiriwa:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe amehitimu Shahada ya kwanza au ya Pili katika fani ya Mechanical Engineering au Energy Engineering au Production Engineering au Mechatronics Engineering au  Electromechanical  Engineering kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na G.P.A isiyopungua 3.5.
 • Uzoefu wa kusomesha na ujuzi wa kutumia kompyuta ni sifa ya ziada.

 

 1. KUJAZA NAFASI TUPU KWA MKUFUNZI DARAJA LA PILI AU MWANDAMIZI DARAJA LA PILI KATIKA FANI YA COMPUTER ENGINEERING NAFASI MOJA (1).

     Sifa za kuajiriwa:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe amehitimu Shahada ya kwanza au ya Pili katika fani ya Computer Engineering kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na G.P.A isiyopungua 3.5.
 • Uzoefu wa kusomesha na ujuzi wa kutumia kompyuta ni sifa ya ziada.

 

3. KUJAZA NAFASI TUPU KWA FANI YA UDEREVA DARAJA LA III NAFASI MOJA (1)

Sifa za kuajiriwa:

 • Muombaji awe mwenye cheti cha elimu ya lazima, na cheti cha udereva na kupata leseni daraja (D) ya gari na kuendelea kutoka katika Taasisi inayotoa leseni na kutambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na uzoefu wa kazi usiopugua miaka mitatu (3).
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 1. KUJAZA NAFASI TUPU YA MLINZI DARAJA LA III NAFASI MOJA (1)

Sifa za kuajiriwa

 • Kuajiriwa mwenye cheti cha elimu ya lazima au awe amefaulu mafunzo ya ulinzi (JKU/JKT/Mgambo au yanayolingana kutoka katika Taasisi inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Muombaji asizidi umri wa miaka 35.
 • Awe Mzanzibar.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 1. NAFASI MPYA MKUFUNZI DARAJA LA PILI AU MWANDAMIZI DARAJA LA PILI NAFASI TATU (3) KWA FANI YA UHANDISI UJENZI NA USAFIRISHAJI

Sifa za kuajiriwa:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe amehitimu Shahada ya kwanza au ya Pili katika fani ya Civil engineering au High way Engineering, au Architecture, au Quantity Surveying and Construction Economic, au Geomatics (land Surveying) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na G.P.A isiyopungua 3.5.
 • Uzoefu wa kusomesha na ujuzi wa kompyuta ni sifa ya ziada.

 

 

 

 

 1. MKUFUNZI AIRCRAFT MAINTENCE ENGINERING DARAJA LA PILI AU

MWANDAMIZI DARAJA LA PILI NAFASI MOJA (1)

     Sifa za kuajiriwa:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe amehitimu Shahada ya kwanza au ya Pili katika fani ya Aerounatics Engineering au Aircraft Maintenenace Engineering au Aerospace Engineering au Avionics. G.P.A isiopungua 3.5, kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Uzoefu wa kusomesha na ujuzi wa kutumia kompyuta ni sifa ya ziada.

 

 1. MKUFUNZI  MWANDAMIZI DARAJA LA PILI FANI YA UHANDISI UMEME  NAFASI MOJA (1)

 

     Sifa za kuajiriwa:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Shahada ya pili katika fani ya Electrical Engineering au Electrical and Electronic Engineering.
 • G.P.A isiopungua 3.5, kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Uzoefu wa kusomesha na ujuzi wa kutumia kompyuta ni sifa ya ziada.

 

 

NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI.

Muombaji anatakiwa andike barua ya maombi na kuiambatanisha na mambo yafuatayo:

 1. Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo.
 2. Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
 3. Picha moja ya muombaji (passport size).
 4. Nambari ya simu na,
 5. Kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibar mkaazi.
 6. Maelezo binafsi (C.V) pamoja na kipengele cha wadhamini wasipungua watatu.

              MAMBO YA KUZINGATIA KWA MUOMBAJI.

 1.  Muombaji atakaewasilisha ‘’Statement of result’’ au ‘’Progressive report’’ maombi yake hayatazingatiwa.
 2.  Muombaji anatakiwa ainishe nafasi moja anayoiomba kati ya kazi zilizotajwa hapo juu. vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa.
 3.  Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na kwa lugha ya Kiswahili.
 4.  Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni siku ya Jumanne ya tarehe 20/10/2020 baada ya kumalizika kwa saa za kazi.
 5. Mawasilino yatafanywa kwa wale tu watakaopita katika mchujo wa awali yaani (short listed).
 6. Maombi yawasilishwe Masjala ya  Taasisi ya Karume  kwa anuani ifuatayo:

MKURUGENZI,

TAASISI YA KARUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA,

S.L.P. 467,

ZANZIBAR.

     Tangazo hili pia linapatikana katika ubao wa Matangazo uliopo KIST.

Ahsanteni

 

BY UTAWALA

 

09/10/2020

Related Posts you may like