KIST WAPOKEA UGENI KUTOKA MAREKANI.

2023-09-25 04:30:15 category

Wawakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la uwekezaji rasilimali watu (GFP), linalojishuhulisha na masuala ya uchomeaji (Welding) Kutoka Nchini Marekani wamefika katika  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), kwa lengo la kuweka ushirikiano   katika elimu ya ufundi.

GFP inalengo la kuanzisha kituo cha umahiri wa uchomaji vyuma ili kuzalisha wataalamu wanaotambulika kitaifa na kimataifa katika nyanja ya uchomeaji vyuma (Certified Welding Engineer).

Pia walipata fursa ya kutembelea workshop mbalimbali za Taasisi ili kujionea vifaa  vya kufundishia.